entrepren

Entrepreneurship/Ujasiliamali, 26th – 28th March, 2019

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kina historia ndefu na ya kujivunia hasa ushiriki wake katika kuendeleza jumuiya ya wafanyabiashara na uchumi wa Tanzania. Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1965, kikiwa chombo huru chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Hadi sasa chuo kina kampasi nne ambazo ni Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya.
Chuo kina kitengo cha Ujasiriamali kilichoanzishwa mwaka 2002. Kilianzishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo, ushauri na kufanya tafiti zinazolenga katika kutoa msukumo na mwongozo kwa wajasiriamali wote. Hii ni pamoja na sekta binafsi na isiyo rasmi katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya kijamii na hivyo kupunguza umaskini na kutoa ajira kwa kushiriki kuendesha sekta binafsi ambayo ina uwezo mkubwa katika kukuza uchumi.
Ili kuweza kufanikisha hayo kituo kinatoa mafunzo yafuatayo kwa pamoja:-

Mafunzo ya Ujasiriamali
Hapa tutajifunza dhana ya ujasiriamali yaani maana, sifa ya mjasiriamali, faida ya mjasiriamali, wazo la biashara, fursa ya biashara na changamoto za ujasiriamali.

Kumbukumbu za Fedha
Wahenga walisema “Mali bila daftari hupotea bila taarifa” kwa kuzingatia hilo kutakuwa na mafunzo ya namna bora ya kuwa na daftari la fedha, daftari la wadaiwa, daftari la bidhaa, daftari la mali, hati ya malipo, stakabathi ya fedha na leja kuu. Lengo ni kumfanya mjasiriamali ataambue mali aliyo nayo na mtiririko mzima wa fedha zake ili aweze kudhibiti mali na mapato yake.

Masoko
Biashara ni kujitangaza hivyo tunatoa mafunzo ya namna ya kutambua soko, namna ya kumfikia mteja, njia bora ya kutambua hitaji la soko, namna bora ya kutangaza bidhaa yako, namna bora ya kupanga bei na mahali pa kufanyia biashara.

Hitimisho
Tunaamini kuwa kwa kupata mafunzo; dhana ya ujasisriamali, namna bora ya kutunza fedha na mali uliyonayo na jinsi kutangaza biashara yako kutafanya biashara yako iwe ya ushindani na yenye tija.

Mbinu za Ufundishaji
Kwa kutambua kuwa wajasiariamali ni watu wanaojitambua na wana malengo makubwa na halisia mbinu zifuatazo zitatumika; majadiliano, kubadilishana uzoefu, kualika Wajasiriamali wazoefu kuelezea uzoefu wao na mbinu mbalimbali wanazotumia kupata mafanikio zaidi. Mwisho kila mshiriki atapata fursa ya kuonyesha jinsi atakavyo jumuisha mafunza haya na biashara yake ili kuongeza tija.

Haki za Mshiriki
Mshiriki atakuwa na haki ya kupata kiti na dawati vyote vya kisasa kabisa, stationaries, kusikilizwa, kujibiwa maswali yake na kutoa maoni na cheti. Nyongeza ni vitafunwa na vimiminika bora kabisa.

Tarehe ya Mafunzo.
Mafunzo haya yatakuwa ya siku tano: Kuanzia tarehe 26 – 28/3/2019.

Mahali
Mafunzo hayo yatafanyika Chuo cha Elimu ya Biashara, Kampasi ya Dar es Salaam.

Gharama
Gharama ya mafunzo ni Sh 200,000/= kwa kila mshiriki. Gharama hizi ni pamoja na dhara za kufundishia, ukumbi, chakula na vinywaji pamoja na cheti. Washiriki watatakiwa kujigharamia usafiri, malazi na matibabu itakapohitajika. Malipo yote yafanyike kupitia Benki ya Posta; yaani TANZANIA POSTAL BANK: Akaunti namba (Account Number) 191504001632, Jina la Akaunti (Account Name): ASSOCIATION CBE CONSULTANCY BUREAU

Mawasiliano
Ndugu. Ngussa Kinamhala 
MKUU WA KITENGO CHA UJASILIAMALI 
Chuo cha Elimu ya Biashara
S.L.P 1968, Dar es Salaam
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Nukushi #: +255-22-2150122
Simu: +255-746 832273

Ndugu. Manongi Ntimbwa
MKUU WA KITENGO CHA UDHIBITINA USIMAMIZI WA UBORA
Chuo cha Elimu ya Biashara 
S.L.P 1968, Dar es Salaam
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Nukushi #: +255-22-2150122
Simu: +255-754312072

 

Social Media Pages

//Copyright © 2019 College of Business Education. All Right Reserved.