Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)-mshindi wa tuzo ya chuo bora cha mwaka 2016 Tanzania, anawakaribisha waombaji (applicants) wenye sifa za kujiunga na chuo muhula mpya wa masomo mwezi wa Machi, 2018 na mwezi Septemba 2018 kwa programu za kutwa na jioni katika ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika kozi mbalimbali.

Programu hizi zinatolewa katika kampasi zote za chuo kama ifuatavyo:

A.     ASTASHAHADA (CERTIFICATE PROGRAMMES) NTA LEVEL 4 (MWAKA 1)

1.   Uhasibu (Accountancy)

2.   Usimamizi wa Biashara (Business Administration).

3.   Masoko (Marketing)

4.   Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management)

5.   TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) (Dsm na Dodoma Pekee)

6.   Mizani na Vipimo (Certificate in Metrology and Standardization) (Kwa Dsm Pekee) 

Sifa za Kujiunga

1.     Mwombaji awe amemaliza kidato cha NNE (IV) na kupata ufaulu wa angalau masomo 4 kwa kiwango cha kuanzia D (4D’s). 

Zingatia: Muombaji wa kozi ya Uhasibu anapaswa awe amefaulu (Form IV) Hesabu kuanzia  kiwango cha D. Na anaeomba Kozi ya Mizani na Vipimo awe amefaulu Hesabu au Fizikia kuanzia  kiwango cha D.

AU

2.     Awe amesoma na kuhitimu NABE II kwa ufaulu wa angalau alama 4

Ada ya Masomo

Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 920,000/= isipokuwa kwa kozi ya TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) ambayo ada yake ni Tshs. 1,220,000/= na Mizani na Vipimo (Certificate in Metrology and Standardization) ambayo ada yake ni Tshs. 853,000/=

B.     STASHAHADA (DIPLOMA PROGRAMMES) NTA LEVEL 5 – 6 (MIAKA 2)

1.   Stashahada ya Uhasibu (Diploma in Accountancy)

2.    Stashahada ya Usimamizi wa Biashara (Diploma in Business Administration)

3.   Stashahada ya Ununuzi na Ugavi (Diploma in Procurement and Supplies)

4.   Stashahada ya Masoko (Diploma in Marketing)

5.   TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) (Dsm na Dodoma Pekee)

6.   Mizani na Vipimo (Diploma in Metrology and Standardization) (Dsm Pekee)

Sifa za Kujiunga

1.     Mwombaji awe amemaliza kidato cha SITA (VI) na kupata ufaulu wa angalau Principal Pass Moja au Subsidiary Mbili katika masomo unganishwa (Combination subject). AU 

2.     Awe amesoma na kuhitimu Astashahada (Certificate) kutoka chuo kinachotambulika na NACTE katika fani zifuatazo:

· Usimamizi wa Biashara (Business Administration).

· Masoko (Marketing)

· Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supplies Management)

· TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT)

Ada ya Masomo

Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 1,100,000/= isipokuwa kwa kozi ya TEHAMA (Information, Communication and Technology (ICT) ambayo ada yake ni Tshs. 1,400,000/= na Mizani na Vipimo (Diploma in Metrology and Standardization) ambayo ada yake ni Tshs. 1,014,400/= 

C.     STASHAHADA YA UZAMILI (POSTGRADUATE DIPLOMA PROGRAMMES)

1.   Postgraduate Diploma in Project Management (PGDPM) – Mwanza pekee

2.   Postgraduate Diploma in Business Administration PGDBA) – Mwanza pekee

3.   Postgraduate Diploma in Human Resource Management (PGDHRM) – Mwanza pekee

4.   Postgraduate Diploma in Financial Management (PGDFM) – Mwanza pekee

5.   Postgraduate Diploma in Investment (PGDIn) – Mwanza pekee

 Ada ya Masomo:

Ada ya masomo kwa Mwaka ni TZS 1,800,000/=

Sifa za kujiunga na Postgraduate Diploma (PGD)

1.      Mwombaji awe amehitimu Shahada (Degree) au Stashahada ya juu (Advanced Diploma). AU

2.     Mwombaji awe na CPA au CPSP

D.      UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI/KUJIUNGA NA CHUO

Maombi yote ya kujiunga na chuo yanafanyika chuoni au kwa njia ya mtandao (Online Application) kupitia tovuti ya chuo www.cbe.ac.tz kwa gharama ya TZS 10,000 tu.

Chuo kimepata kuwa chuo bora cha mwaka kwa mwaka 2016. Njoo ujiunge na chuo bora kwa elimu bora.

ZINGATIA:

Ada italipwa kwa awamu nyingi kama itakavyo elekezwa. Hostel zipo kipaombele kitatolewa kwa watakaowahi kuja kuanza masoma.

 

E.     MAHALI TULIPO

1.     Dar es Salaam

Bibi Titi Mohamed Street, S. L. P. 1968, Dar es Salaam

Simu : +255-22-2150177/255-22-150610                             

Fax No: +255-22-2150122

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Website: www.cbe.ac.tz.

2.     Dodoma

Eneo la Makole pembezoni mwa barabara iendayo Dar es Salaam

S. L. P. 2077, Dodoma

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Au Piga Simu: +255 26 2321200

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

3.     Mwanza

Chuo kipo mjini - Mtaa wa stesheni, Mkabala na Maktaba ya Mkoa (Roundabout ya Samaki) pia tuna Kampasi mpya Kaangaye-Nyakato (km 10 kutoka mjini)

Kwa mawasiliano zaidi piga simu +255 767 692 558, AU +255 712 521 349, AU+255 684 525 338 AU

Tuma ujumbe kupitia Barua Pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. AU fika   chuoni uchukue fomu ya kujiunga.

 4.     Mbeya

Chuo kipo Forest ya Zamani kilipo Chuo Kikuu Huria (Open University).

Kwa mawasiliano Zaidi Piga Simu: +255 744 762 825 AU

Tuma ujumbe kupitia Barua Pepe: Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. AU Fika chuoni

Apply now

Follow us on social media

Copyright © 2018 , College of Business Education. All Right Reserved.