CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA
KAMPASI YA MBEYA
FURSA YA KITAALUMA KWA WAKAZI WA NYANDA ZA JUU KUSINI


Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya kilianzishwa Julai 1, 2013 kwa lengo la kuwasogezea huduma wakazi wa nyanda za juu kusini (mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Njombe, Katavi na Rukwa), na kuwapunguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kwenye kampasi zingine za chuo hiki ambazo zipo mbali na ukanda huu.
Chuo ni cha Serikali chini ya Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, na kinatoa mafunzo katika nyanja za Usimamizi wa Biashara, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, na Masoko. Mafunzo yanatolewa katika ngazi ya Astashahada(Basic Certificate) na Stashahada (Ordinary Diploma). Kozi hizi ni mahususi kabisa kwa wahitimu wa kitado cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) wenye lengo la kupata weledi na maarifa katika fani hizi za biashara.  


Kampasi inatoa Mafunzo kwa Kozi zifuatazo:
1)    Astashahada ya Usimamizi wa Masoko
2)    Astashahada ya Uhasibu
3)    Astashahada ya Usimamizi wa Biashara
4)    Astashahada ya Ununuzi na Ugavi  
5)    Stashahada Usimamizi wa Masoko
6)    Stashahada ya Uhasibu
7)    Stashahada ya Usimamizi wa Biashara
8)    Stashahada ya Ununuzi na Ugavi  


 
Kampasi ya Mbeya Ndio Mahali Sahihi kwa kupata Elimu ya Biashara
Katika ulimwengu wa leo uliogubikwa na utitiri wa vyuo, ikiwemo kanda hii ya nyanda za juu kusini, ni jambo la busara kwa wanafunzi na hata wazazi kwa ujumla kujua mapema ni vyuo gani vinavyowafaa vijana wao kufanya masomo yao ya elimu ya juu.

Ni jambo la busara kujiuliza kwa nini mtu mwenye nia ya kupata stadi na maarifa katika fani za biashara asome Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Mbeya. Zifuatazo ni baadhi ya sababu za msingi zinazompa mtu imani ya kujiunga na Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Mbeya:-


1.    Tuzo ya Ubora kwa Upande wa Vyuo vya Elimu ya Juu: Hivi karibuni CBE imepokea tuzo ya uongozi bora (Tanzania Leadership Awards 2016). Hii inadhihirisha kwamba kwa upande wa vyuo vya elimu ya juu, CBE inatambulika katika mchango wake wa kukuza na kuendeleza sekta ya biashara katika Taifa letu.  


2.    Kukua katika nafasi za kitaaluma (academic ranking): Ikilinganishwa na vyuo vya elimu ya juu vingine nchini Tanzania. CBE imekuwa ikipanda daraja katika nafasi za kitaaluma. Kwa mfano, katika nafasi za kitaaluma kwenye tovuti ya Webometrics (http://www.webometrics.info/en), kati ya vyuo 51 vilivyopo nchini, CBE imekuwa ikipanda daraja toka nafasi ya 23 kwa mwaka 2014 hadi nafasi ya 22 mwaka 2015.  Na kwa mwaka huu wa 2017 CBE inashikilia nafasi ya 17.  


3.    Makusudio ya kuanzishwa kwake: CBE ilianzishwa mahususi na serikali ya Tanzania ili kuzalisha wataalam wa biashara. Siku hadi siku Chuo kimekuwa kikiendelea kutoa wataalam mahiri katika nyanja za biashara.


4.    Miundo mbinu ya kujifunzia. Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya inayo miundo mbinu ya kujifunzia (learning infrastructure) inayoendana na mahitaji ya jamii ili kumwezesha mwanafunzi kupata elimu bora. Hii ni pamoja na kompyuta za kujifunzia na maktaba nzuri yenye huduma ya mtandao (internet).  


5.    Mitaala: Chuo cha Elimu ya Biashara hupitia mitaala yake mara kwa mara kwa lengo la kuiboresha ili kukidhi uhitaji wa soko na mazingira. Kwa mfano kwa mwaka wa masomo uliopita (2016/17) chuo kimeweza kuipitia mitaala yake na kuiboresha zaidi na itaanza kutumika mwaka huu wa masomo wa 2017/18.

Kwa ujumla, Chuo cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Mbeya ni fursa tosha ya kupata elimu ya biashara kwa wakazi wa nyanda za juu kusini. Chuo kipo Forest ya Zamani kilipo Chuo Kikuu Huria (Open University).


UDAHILI UNAENDELEA, TEMBELEA TOVUTI YETU (www.cbe.ac.tz) KUPATA MAELEZO YA NAMNA YA KUJIUNGA. AU FIKA CHUONI MOJA KWA MOJA ILI KUCHUKUA FOMU ZA KUJIUNGA NA KISHA KUJISAJILI.


Au Piga Simu: +255 744 762 825
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


KARIBU CBE MBEYA

Social Media Pages

Copyright © 2018 , College of Business Education. All Right Reserved.