Mariam Albert’s & Eva Lyimo's PPP Story

Rate this item
(6 votes)
Mariam Albert’s & Eva Lyimo's PPP Story

Mariam Albert is in her second-year of a Diploma in Marketing at the College of Business Education (CBE) in Dar es Salaam campus. Her aim is to become a Marketing manager of a multinational company. When she enrolled, Mariam missed the opportunity to live in a hostel at the campus as is small and can only accommodate a handful of students. Her family lives in a region far from Dar es Salaam – so she had to look for a room to rent off-campus. Mariam was able to find a room in a house many streets away from the campus.

But Mariam is facing a lot of challenges staying off-campus. Traffic is a constant problem as she goes to and from college. She is spending a lot of money on her daily expenses - paying rent, water and electricity bills and bus fares every day to and from college. Mariam knows that many female students like herself are concerned for their safety, both as they travel to and from the college and even while in the strange apartment. She knows all the pressure from her new accommodation interferes with her concentration on her studies and achieving here aim of a good job in the future.
One afternoon as Mariam was having lunch at the College's canteen, she joined a conversation that her friends and some canteen workers were having. They were discussing the proposed on-campus hostel being prepared as a Public Private Partnership (PPP) project. The project was being presented to the off-campus students and the canteen owners and other community members. They spoke of how the new hostel could change the campus outlook, improve students' welfare and safety, increase business opportunities for canteen owners, and other small businesses around the campus. Everyone seemed excited and looking forward to the start of construction.

After lunch, Mariam called her mother and told her of the exciting news. Her mother was so happy and relieved. She told Mariam how she is always worried about her safety in the crowded city with no relatives, challenging public transportation - especially after college hours, thinking she may get home late at night due to traffic. She just hopes the new accommodation will be safe and a good place for her daughter to study. Mariam was touched by her mother's words.

As a result of the engagement with community members like Mariam, CBE knows how to ensure the student hostel can provide a safe and affordable housing option for its students.
PPPs are being prepared for communities across the country as a step towards Tanzania’s Development Vision 2025. One way PPPs are being used is to provide better and safer student hostels for those young women and men pursing further education. A priority is to help young women feel more secure and able to focus on learning. The project management team for CBE’s Dar es Salaam’s campus, led by the college under the guidance of the Minister of Finance, has consulted many community members just like Mariam over the past year. Their aim is to understand the needs of the community and to ensure that the PPP project they are preparing will meet these needs. This story is one example of who the PPP is being prepared to help and how it will improve their lives. The project management team will continue to engage with communities as they move towards procurement of the private partner, then throughout construction and the operation of the hostel.

Hadithi ya PPP ya Eva Lyimo

Eva Lima anaishi na wazazi wake mtaa wa Kimara Mwisho, Dar es salaam. Eva anaishi umbali wa kilomita kumi na nane kutoka Chuo cha Usimamizi wa Biashara (CBE), tawi la Dar es Salaam anakosomea Ugavi ngazi ya Stashahada. Imekuwa kawaida kwake kupita katikati ya mitaa ya jiji iliyo na shughuli nyingi sana, na hali huwa mbaya kwake muhula wa masomo ukianza. Hulazimika kukatisha usingizi ili awahi kuamka na kuwahi usafiri wa kwenda chuoni akitokea Kimara. Kutokana na changamoto ya usafiri Eva hujihimu mapema sana kwenda kituo cha Mwendokasi cha Kimara kwa ajili ya kuepuka kusongamana na kugombania usafiri.

Kama inavyokuwa asubuhi anapokuja chuoni, Eva husubiri kwa hamu mhadhiri wa kipindi cha mwisho ahitimishe nukta yake darasani ili aharakishe kwenda kituoni kugombania kuingia tena kwenye Mwendokasi kurudi zake Kimara. Huwa anaumia moyoni anapowaaga marafiki zake waliobahatika kubaki chuoni. Akiwa katika kituo cha Mwendokasi, itamchukua Eva muda mrefu kupata basi na hutumia takribani saa moja kufika nyumbani.

evaweb
    Photo: Eva Lema

Anapokuwa kituoni akisubiri usafiri, anafikiria jinsi marafiki zake walivyo na bahati ya kupata nafasi katika hosteli chuoni. Anakumbuka ahadi ya ujenzi wa hosteli mpya ndani ya eneo la chuo na anatamani litokee mapema ili anufaike na fursa hiyo ya kuishi ndani ya chuo. Eva anatamani ikamilike hata kesho kwani ataweza kufika darasani kwa wakati huku akiwa makini na masomo na akili iliyotulia. Mara nyingi amekuwa akikosa furaha kwasababu ya kuwaza mateso ya kusafiri kila siku asubuhi na jioni.  Akiishi kwenye hosteli za chuo atakuwa salama zaidi kwani ataepuka hatari za kutembea usiku akitoka chuo.

Lahaula, kumbe muda wote huo akiwa amezama katika lindi la mawazo kuhusu taarifa aliyosikia ya mipango ya ujenzi wa hosteli, mara ghafla anasukumwa na watu waliokuwa wanakimbilia basi la mwendokasi ambalo hakuliona au kulisikia. Ah! Ameshakosa nafasi na limejaa hadi mlangoni.

Basi jingine likaja naye alibahatika kulipanda. Akiwa amesimama kwenye basi, mkono wake ukishikilia bomba juu yake, anawaza kama angeweza kupata nafasi katika mradi wa hosteli za ndani ya chuo unaoandaliwa na CBE. Anajua chuo kinaandaa mradi huo kama Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili kuwasaidia wanafunzi wanaoishi nje ya chuo. Eva alishiriki kwenye mahojiano kuhusu ujenzi wa hosteli hizo mpya za PPP. Alifurahi sana na anaombea hosteli hizo zijengwe na wanafunzi wapangishwe kwa gharama nafuu kwani itakuwa imempa unafuu kwake na kwa wanafunzi wengine wenye changamoto kama zake. Alifurahishwa pia alipojua kwamba mikataba ya PPP itahakikisha majengo yanasimamiwa na kutunzwa kitaalamu.

PPP zinaandaliwa kwa ajili ya jamii mbali mbali nchini kama sehemu ya Dira ya Maendeleo Tanzania ya mwaka 2025. Kwa kupitia PPP hosteli bora na salama zinajengwa kwa ajili ya wanafunzi wa kike na wa kiume ili waweze kujiendeleza vizuri kimasomo. Kipaumbele ni kuwasaidia wanafunzi wa kike wasome na kuishi katika mazingira salama. Mwaka uliopita, timu ya usimamizi wa mradi wa CBE, tawi la Dar es Salaam, ikiongozwa na chuo, chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha ilifanya mazungumzo na wanajamii wengi kama Eva. Lengo likiwa kutaka kuelewa mahitaji ya jamii na kuhakikisha kwamba mradi huo wa PPP unaotengenezwa utakidhi mahitaji hayo. Hadithi hii ni mfano mmojawapo wa namna mradi huu wa PPP unavyoweza kuwasaidia walengwa na kuboresha maisha yao. Timu ya usimamizi wa mradi itaendelea kushirikisha jamii katika mchakato wa kutafuta mshirika kutoka sekta binafsi, kisha wakati wote wa ujenzi na usimamizi wa hosteli.

History of CBE

The COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (CBE) was established in 1965 by the Act of the Parliament. COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION Act No. 31 of 1965. His Excellency, J.K. Nyerere, the first President of the United Republic of Tanzania officially opened the new College in January 1965. The College was officially named the “College of Business Education” (CBE). The said Act of Parliament gives the College its legal status as an autonomous institution with its Governing Body. The College shall be governed and administered in accordance with the provisions of this Act.

CONTACT US

The origin of the College of Business Education (CBE) is closely linked to the history of the Nation itself.

Address : Bibi Titi Mohamed Rd. P. O. Box 1968, Dar es Salaam

Hotline : +255-022-2150177

light arrowWELCOME OUR FIRST YEARS TO CBE, WE WISH YOU NICE STUDIES