Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) anakaribisha maombi ya kujiunga na Chuo katika kampasi za Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya kwa masomo yatakayoanza mwezi MACHI 2025 katika ngazi za Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) na Shahada ya Umahiri (Mastesrs Degree). Mfumo wa ufundishaji utakuwa ni usomaji kwa njia ya Mtandaoni (Online Learning System).
Postgraduate Diploma (Stashahada ya Uzamili) Muombaji awe amemaliza Degree ya kwanza (Bachelor Degree) katika ufaulu wowote Au awe amemaliza Stashahada ya juu (Advanced Diploma) kutoka Katika chuo kinachotambulika na TCU au NACTVET.
Shahada ya umahiri (Master’s Degree): Muombaji awe amemaliza Degree ya kwanza na ufaulu wa angalau Lower second-class au Postgraduate Diploma kutoka Katika chuo kinachotambulika na TCU au NACTVET.
Mwisho wa kupokea maombi kwa ajili ya kujiunga na Chuo ni 10/03/2025.
Waombaji watume maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Chuo www.cbe.ac.tz Au fika katika kampasi zetu. Gharama za maombi ya kujiunga na chuo ni BURE.
Ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia
Barua pepe: admission@cbe.ac.tz Huduma Kwa Wateja: 0222 211 560
Kwa Dar es salaam Simu Namba: 0777 151 323
Kwa Dodoma Simu Namba: 0734 330 104 au 0692 659 357
Kwa Mwanza Simu Namba: 0659 707 000 au 0767 692 558
Kwa Mbeya Simu Namba: 0674 415 629 au 0769 525 293
Tovuti: www.cbe.ac.tz
WOTE MNAKARIBISHWA.